Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Simba imebadilika! Ni kauli ya Kocha Mkuu wa Timu Hiyo, Pablo Franco , Alia na Washambuliaji

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Simba imebadilika! Ni kauli ya kocha mkuu wa timu hiyo, Pablo Franco ambaye amesema tangu amekichukua kikosi hicho timu imeimarika, lakini amelia na eneo la ushambuliaji.


Pablo alisema amefanikiwa kulifanya eneo la ulinzi kuwa imara akitolea mfano nyota wake walivyocheza dhini ya Yanga.


“Sehemu nyingine ambayo imebadilika kwenye kikosi chetu katika kila mechi tumekuwa na wastani mkubwa wa kutengeneza nafasi za kufunga, lakini bado tunaendelea kuboresha kwenye kumalizia kwani tunatengeneza nafasi nyingi tunatumia chache.”


“Simba inayoonekana wakati huu baada ya muda zaidi itaimarika kucheza katika soka la chini la kuvutia, pasi kuanzia nyuma hadi bao kufunga mabao na muda mwingine kushambulia kwa haraka.”


Pablo amekiongoza kikosi cha Simba katika mechi tano za michuano yote hadi sasa tangu apewe mikoba ya kuifundisha akizikabili Ruvu Shooting, Red Arrows (mara mbili), Geita Gold na Yanga.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments