CAF yamkingia Kifua Mwamuzi Sikazwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetupilia mbali rufaa ya Tunisia juu ya mchezo wao dhidi ya Mali kwenye michuano ya Afcon kundi F kumalizwa mapema kabla ya dakika 90 kuisha ,mchezo uliochezeshwa na mwamuzi Mzambia Janny Sikazwe na kumalizika  kwa Mali kuibuka na ushindi wa 1-0.

Katika taarifa ya CAF, waliyoitoa mapema leo, wamesema  kamati ya mashindano ya CAF iliyokaa siku ya Alhamisi imeyatupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na chama cha soka nchini Tunisia (FTF) huku kukiwa hakuna  maelezo ya ziada  juu ya kutupiliwa mbali kwa rufaa hiyo

Upande wa FTF , Mapema siku ya Alhamisi kupitia tovuti ya chama cha soka nchini Tunisia (FTF)  walitoa taarifa kupitia kwa Hussein Jenaieh  ikisisitiza “Tutafanya chochote  ili kulinda haki ya timu yetu ya taifa ,sisi sio watoto wadogo”.

Afisa mwamuzi wa CAF Essam Abdul Fattah aliviambia vyombo vya habari vya Misri kwamba  mwamuzi alipigwa na jua hali iliyoathiri maamuzi yake katika mchezo huo "Baada ya mchezo, alihitaji kwenda hospitali kwa sababu hali ya hewa ilikuwa ya joto sana" amesema Fattah

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad