Mrithi wa Ndugai: CCM yasogeza vikao mbele

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesogeza mbele vikao vyake kikiwamo cha kamati kuu kutoka jana Jumanne, tarehe 18 Januari 2022 hadi kesho Alhamisi, jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ratiba ya awali ya vikao hivyo vyenye lengo la kuchakata na kumpata mrithi wa Job Ndugai, aliyejiuzulu nafasi ya spika wa Bunge la Tanzania, tarehe 6 Januari 2022, ilikuwa vinafanyika kwa siku mbili yaani jana na leo Jumatano.

Jumla ya wagombea 70 wamejitosa kuwania nafasi hiyo ya uongozi wa muhimili wa Bunge.

Leo Jumatano, tarehe 19 Januari 2022, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamud Shaka ametoa taarifa kwa umma kikao cha kamati kuu kitafanyika tarehe 20 Januari, 2022 badala ya tarehe 18 Januari, 2022 katika ofisi za Makao Makuu (White House), Dodoma.


 
           
“Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Maandalizi ya vikao vyote hivyo yamekamilika,” amesema Shaka

Kikao hicho cha kamati kuu, kitakuwa na jukumu zito la kuwafyeka wagombea 67 kati ya 70 waliojitosa kwenye kinyanyany’iro hicho na kubaki na majina matatu ambayo yatapelekwa katika kamati ya wabunge wa CCM.


Kamati ya wabunge wa CCM, itakuwa na jukumu la kumchagua mmoja ambaye atakwenda kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi wa spika utakaofanyika tarehe 1 Februari 2022, siku ya kwanza ya mkutano wa kwanza wa Bunge la sita.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad