Serikali yahakiki mkataba Bandari ya Bagamoyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali inapitia mkataba wa mradi wa uwekezaji wa ukanda maalumu wa Bagamoyo, ili kuhakikisha unakuwa na tija kwa masilahi ya Taifa.

Juni 24 mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Hata hivyo, Rais wa tano, hayati John Magufuli aliwahi kukaririwa akisema ujenzi wa mradi wa Bagamoyo una masharti magumu ya mwekezaji ndio sababu ya kusuasua kutekelezwa.

Miongoni mwa masharti hayo ni baada ya ujenzi huo kukamilika, Tanzania haitaruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine yoyote Pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia Tanga mpaka Mtwara.


 
Juzi, katika mkutano wake na wanahabari wa mkoa wa Njombe, Msigwa aliulizwa msimamo wa Serikali kuhusu mchakato huo umefikia wapi. Katika majibu yake, alisema, “kama nchi haiwezi kuingia mikataba isiyokuwa na manufaa kwa Taifa. Kazi inayoendelea sasa ni kupitia mkataba pamoja na kuangalia masilahi ya Taifa yako wapi na mwekezaji. “Si kweli kwamba Bandari ya Bagamoyo haina tija na Serikali haijawahi kutamka. Majadiliano yakikamilika Serikali itaeleza kinachoendelea kuhusu mradi wa Bagamoyo,” alisema.

Msigwa aliyewahi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, alisema mradi wa Bagamoyo unajumuisha ujenzi wa viwanda zaidi ya 1,000, nyumba za makazi, maeneo maalumu ya viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi.

“Huu ni mradi mkubwa lazima Serikali iungalie vizuri, ili kuhakikisha masilahi ya Taifa yanalindwa,” alisema Msigwa. Pia alizungumzia mradi wa Liganga na Mchuchuma, akisema kiuhalisia ulitakiwa kuanza kwa kuwa mwekezaji alishapatikana, lakini hakuanza kutokana na masuala mbalimbali kujitokeza.


Alisema wakati wa kuutekeleza mradi huo, umefika na kwamba sasa majadiliano na mwekezaji yenye sura mbili yanaendelea. Msigwa alisema majadaliano hayo yanalenga lini utekelezaji wake utaanza.

“Naomba nisiseme lini mradi utekelezaji unaanza, lakini tambueni mambo ni moto. Endapo mwekezaji atashindwa kuendeleza mradi huu, Serikali ipo tayari kumtafuta mwingine, tunataka chuma cha Liganga na makaa ya mawe,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad