Petit Man "Familia Ndiyo Kila Kitu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MENEJA wa wasanii mbalimbali nchini Tanzania, Hemed Manungwi almaarufu Petit Man anasema kuwa, hakuna kitu kinachompa furaha hivi sasa kama akiwa na familia yake; yaani mkewe na mtoto wake wa kiume kwani kunamfanya asahau shida zote alizopitia huko nyuma.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Petit Man anasema kuwa, anafurahi anapokuwa na majukumu kwa familia yake ambayo anaipenda ndiyo maana huwezi kumkuta sehemu bila kuwa na familia yake hiyo pendwa. Pia anasema kutokana na hilo mwili umekuja kwa sababu ya kupendwa na kupenda.

“Huwezi kuamini, mimi nainjoi sana mpaka naona kweli nafurahia kitu ambacho ninacho, naipenda sana familia yangu na kila kukicha ndiyo inanipa furaha na kuniongeza nguvu katika utafutaji wangu na ninajiona nina majukumu kama baba na lazima niyatimize,”
anasema Petit Man ambaye ni mume mstaafu wa mwanamama Esma Platnumz.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad