Walio Tayari Kuhama Ngorongoro Kwa Hiari Kulipiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kwamba serikali itagharamia gharama za wananchi wote wanatakaokuwa tayari kuhama ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari.

Waziri Mkuu amesema hayo wakati akitoa hoja ya kuahirisha bunge jijini Dodoma na kueleza zaidi kwamba suala la kulinda mazingira ni la Watanzania wote.

Kiongozi huyo ambaye amefanya mazungumzo na wakazi wa eneo hilo hivi karibuni amewasihi wale wote walioko tayari kuhama wasikwamishwe na watu wengine.

Amewataka wanaotaka kuhama kujiandikisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mkuu wa Wilaya ya Karatu na Mhifadhi Mkuu ameeleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na watu wote kulinda mazingira ya eneo hilo na maeneo mengine nchini.

Akitilia mkazo suala hilo, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa huo ndio uamuzi wa sasa wa serikali, na kuwataka wananchi kupuuza uzushi kuwa bunge limetunga kanuni za kuwaondoa wananchi hao.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha bunge hadi Aprili 5, 2022 saa tatu asubuhi.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad