Kesi ya maofisa saba wa polisi yatumia dakika mbili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis inayowakabili maofisa saba wa polisi mkoani Mtwara, imeahirishwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Washitakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara leo Jumanne Machi 22, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lugano Kasebele na kutumia dakika 2 tu mahakamani hapo kabla ya kuahirisha hadi Aprili 5, 2022

"Haya tuonane tarehe 5 Aprili upelelezi haujakamilika" Amesema Hakimu Kasebele

Wakili wa Serikali Gidion Magesa ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo, kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa tena.


 
Kesi hiyo  inawakabili maofisa saba wa polisi ambao ni Ofisa Upelelezi Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje,  Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa zahanati ya Polisi, Marco Mbuta.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad