3/17/2022

Miss World 2021 apatikanaKarolina Bielawska mwenye umri wa miaka 23 kutoka nchini Poland amefanikiwa kushinda taji la urembo la dunia Miss World 2021.


Ushindi wa mrembo huyo unamfanya alipokonye taji kutoka kwa Toni-Ann Singh aliyekuwa Miss World 2019 kutoka Jamaica, ambaye ndio mrembo aliyekaa na taji hilo kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu.


Muda unaomuingiza katika historia ya kuwa mrembo wa kwanza kulihodhi taji hilo kwa kipindi kirefu zaidi.


Nafasi ya pili imeshikiliwa na mrembo Shree Saini kutoka nchini Marekani na nafasi ya mshindi wa tatu imeshikwa na mrembo Olivia muwakilishi wa taifa la Ivory Coast.


Shindano hilo limefanyika mapema leo Machi 17, 2022 huko San Juan Puerto Rico.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger