Muna "Sijamzuia Mtu Kufanya Sajari, Ila Kuna Kuoza"Muna Love; ni staa wa Bongo Movies ambaye baada ya kufanikiwa kurekebisha athari alizozipata baada ya kwenda nje ya nchi na kufanyiwa upasuaji wa kuongeza shepu na kuweka dimpozi, amewashauri mabinti wote wenye ndoto za kufanya hivyo basi waache.
Hata hivyo, Muna amesisitiza kuwa hajamkataza mtu ila watakuja kumkumbuka.

“Nikiwaambia madhara nyie ambayo mimi ninayo wala sifichi ila kila surgery ina madhara yake, nitakuja kuongea mwanzo hadi hatua ya mwisho.

“Uzuri hata huko ma-doctor wa Hispania walioniokoa nitawashukuru na nitawatajia na hospitali mkaulizie wenyewe ila ngojeni kwanza nipumue.

“Na sijamzuia mtu asifanye, nenda utakuja kunikumbuka hata ushuhuda wa moyoni mimi ni mhanga na nitawajuza tu.

“Wasichana wengi au baadhi wananifuatilia na kutamani vingine kutoka kwangu, sitaki wapotee na niwe dada mbaya nikikaa kimya natakiwa niwaambie pia kitu kile cha hatari ya kifo au kuoza,” anasema Muna ambaye amerejea Bongo na shepu lake la kuvunja chaga.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad