3/18/2022

Sakata la Steve Nyerere na wasanii lapamba motoWakati kukiwa kumeibuka mjadala wa msanii wa filamu, Steven Mengele maarufu kwa jina la Steve Nyerere kuteuliwa kuwa msemaji wa Shirikisho la Muziki, Shirikisho hilo limefafanua na kumtaja msemaji.
Dar es Salaam. Wakati kukiwa kumeibuka mjadala wa msanii wa filamu, Steven Mengele maarufu kwa jina la Steve Nyerere kuteuliwa kuwa msemaji wa Shirikisho la Muziki (Shimuta), Shirikisho hilo limefafanua na kumtaja msemaji.

Kutambulishwa kwa Steve Nyerere kuwa msemaji wa Shirikisho hilo uliibua mjadala miongoni mwa wanamuziki akiwemo mwanamuziki Diamond Platnum, lakini Katibu Uenezi wa Shirikisho hilo, Siza Mazongera aliyezungumza na Mwananchi leo Machi 18, amesema yeye ndiye msemaji rasmi wa shirikisho na Steve ni mhamasishaji tu.

Akifafanua jambo hilo, Siza aliyewahi kutesa na wimbo wa Segere, amesema kwa mujibu wa katiba yao Katibu uenezi ndio msemaji wa shirikisho na ambaye huchaguliwa kwa kupigiwa kura, ambaye ni yeye.

“Mimi ndio msemaji shirikisho kwa mujibu wa katiba yetu, kwa sababu nilichaguliwa kwenye uchaguzi uliofanyika Aprili 2021 baada ya kugombea na kushinda kwa asilimia 80,” amesema Siza.


 
Amesema walimteua Steve kuwa mhamasishaji kutokana na kuwa na karama hiyo na kubainisha kuwa hilo lilifanyika na kupitishwa na wajumbe wa bodi, kikao ambacho kilifanyika mwezi mmoja uliopita.

“Sioni shida Steve kuwa mhamasishaji wetu, ukweli ni kuwa ana uwezo huo, na ndio maana hata alipotangazwa kuwa msemaji mitandao imelipuka kwa kila mtu kusema lake na imetusaidia hata kujulikana kuwa kuna shirikisho la muziki, nadhani ni mwanzo mzuri,” amesema Siza.

Katika wito wake kwa wasanii na wadau wa muziki, amewaomba wampe muda Steve kuona kama kazi hiyo ataiweza au la na kuongeza kuwa, kutokuwa kwake mwanamuziki hakuwezi kuathiri shirikisho hilo kwa kuwa hata Haji Manara ni mhamashaji wa timu ya Yanga lakini hajawahi kuwa mcheza mpira.


Wasanii walivyompiga Steve

Moto huo wa uteuzi wa Steve ulianza kuzungumziwa juzi, lakini umekolezwa zaidi na msanii Diamond Pltanumz, ambaye kupitia mtandao wa Insta Story yake ameandika aliitahadharisha Serikali kuwa makini na watu wanaoteuliwa kwenye shirikisho hilo.

“Serikali ina nia njema sana ya kukuza Sanaa ila inatakiwa kuwa makini na watu wanaowateua kusimiamia Nyanja mbalimbali katika tasnia zetu maana watu hao wanachokifanya ni kulidhalilisha Taifa na kufafanya lionekane halina weledi,” ameandika Diamond.

Mwingine aliyetoa maoni yake ni mtayarishaji maarufu wa muziki, Joachim Kimaro maarufu kwa jina la Master J, akitaja moja ya sababu anayoona Steve hana sifa ya kuwa msemaji wa tasnia hiyo, ni kutokana na kutokuwa mwanamuziki.

“Yaani ni sawa leo umchukue mtu wa mchezo wa tenesi akampeleka kuwa msemaji wa mpira wa miguu, jambo ambalo sio sahihi,” amesema Master J.

Naye msanii Webiro Wasira maarufu kama Wakazi ambaye naye ameandika kwenye ukurasa wake mtandao wa Instagram akisema, “Steve Nyerere is charismatic & Influential (ana karama na mwenye ushawishi). Ni mtu mzuri (hana baya) ila anakosa vigezo ambavyo ni muhimu zaidi kuliko hiyo Charisma na ushawishi wake.”

Hata hivyo, Katibu wa Shirikisho la Muziki, Farid Kubanda’Fid Q’ ametetea uamuzi hayo na kueleza sababu ya kuteuliwa Steve ni kutokana na kuwa mtu ambaye ukipanga naye jambo linaweza kwenda, ana maono na muelewa licha ya mapungufu madogo madogo aliyonayo.

Tayari shirikisho hilo limesema litatolewa taarifa rasmi kesho Machi 19, 2022.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger