Ticker

6/recent/ticker-posts

Tuzo za Tanzania Music Awards, Kutokuwepo Kwa Wanamuziki wa WCB, Malalamiko Yamekuwa Mengi

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>
BASATA wametoa nominees ambao wanachuana kwenye categories mbalimbali za tuzo za muziki nchini ambazo zinatarajiwa kutolewa weekend ijayo ya tarehe 26 March, malalamiko yamekuwa mengi sana hasa kuhusu WCB kutoonekana kwenye tuzo hizo, kwanza @basata.tanzania inabidi wajitokeze hadharani kusafisha hali ya hewa ili watanzania wajue kwanini hili limejitokeza.

Kama zilivyo tuzo nyingine kubwa duniani kama Grammy, wasanii upeleka kazi zao na kupendekeza categories ambazo wangependa kushindana, jambo ambalo unaweza kuwaelewa BASATA kwenye hili ni kurefer kauli ya Diamond Platnumz aliyoitoa kwenye interview aliyofanya The Switch ya Wasafi FM hivi karibuni kuwa kushindanishwa na wasanii wa Tanzania ni kuwaonea tu,yeye ni wa kushindana na watu wa Level yake.

Hii kauli imejaa majivuno na kujikweza na ni wazi Diamond hakupeleka kazi zake BASATA. Kauli ya Diamond kukosoa mirabaha na kudai Rayvanny alipata mrabaha mkubwa huko nje ni kauli za dharau na kuona nyumbani hakuna lolote, unawawekaje WCB kwenye List ikiwa washajiona ni miamba na wanastahili vikubwa zaidi. Leo hii unataka usawa na watu wa Colombia,bro unajua wameanza lini kuset strategies za kulinda haki za msanii? Diamond anasahau alipewa tuzo 3 za Kili Music hadi akachanganyikiwa hasiamini macho yake,hii leo anavimba.

@basata.tanzania wamekosea kwenye baadhi ya categories mfano, category ya Best Male Bongo Flava musician of the year, si kwa ubaya, Ben Pol ana project gani kubwa aliyofanya mwaka uliopita hadi akae hapo,? Ok tumewatoa WCB, kwenye category kubwa kama hii anakosaje Alikiba? Unamuweka Whozu? Hata kama msanii alipendekeza awepo lakini wangechuja. Kingine kuna uzembe @basata.tanzania ,Lala sio wimbo wa Jux ni wimbo wa Rayvanny,kwanini Rayvanny hasiwepo kwenye tuzo na bado kazi yake mkampa msanii mwingine kuchukulia tuzo?

Kwa mashabiki wa WCB wanaoreact s2kizzy kuwepo kwenye tuzo kupitia wimbo wa IYO, nadhani hapo hakuna tatizo maana producer ndiye mmiliki halali wa beat la IYO na sio msanii,hivyo ni sawa kwake yeye kulitumia kwenye tuzo kama ilivyo kwa madirector.

Hivi @basata.tanzania ni kweli @damiansoulmusic ni upcoming artist? Muombeni radhi mara moja

By Sajo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments