A$AP Rocky Mchumba wa Rihanna maji shingoni, Polisi wakamata Bunduki nyumbani kwake

 


Ripoti ya uchunguzi uliofanywa nyumbani kwa rapa Asap Rocky, hatimaye imetoka, ambapo inadaiwa polisi wamekuta bunduki kadhaa na kitu pekee ambacho hakikuwekwa wazi ni kama Je, polisi waliipata Bunduki halisi iliyotumika kumpiga mtu risasi wakati wa mabishano kwenye tukio lilitokea huko Hollywood au la.


Kwa mujibu wa TMZ, vyanzo vya utekelezaji wa sheria (Law enforcement sources) vinasema wapelelezi watafanya majaribio ya silaha moja baada ya nyingine ili kubaini ikiwa Rocky ndiye mhusika mkuu wa shambulio hilo, pia imedokezwa kuwa polisi watafuatilia historia ya bunduki ili kubaini zilikotoka, nani alizinunua au kama zimeripotiwa kuibwa sehemu yeyote.


Taarifa ya awali ilieleza undani wa namna Rocky alivyokamatwa katika uwanja wa ndege LAX alipokuwa ameshuka katika ndege binafsi wiki iliyopita wakati yeye na Rihanna wanarudi kutoka mapumzikoni huko Barbados.


Rocky alifunguliwa kesi hiyo kufuatiwa kuhusishwa na tukio la kushambulia kwa kutumia silaha, kwa madai ya kuwa aliwafyatulia risasi watu kadhaa na kusababisha taharuki huku mtu mmoja akiripotiwa kujeruhiwa katika sehemu ya mkoni wake mwezi Novemba 2021.


Kwa mujibu wa polisi kiini cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni ugomvi kati ya Rocky na mwenzie waliogombana huko Hollywood na kusababisha milio ya risasi kurindima huku mshukiwa mkuu akiwa ni rapa Asap Rocky.


Rocky na timu yake ya wanasheria wanasema walishangazwa na kukamatwa kwake kwa madai ya kuhusishwa na kesi ya risasi. pia sababu za kutoarifiwa kujisalimisha kwa hiari kiasi cha kuvamiwa ghafla na maafisa usalam ambao walimkamata punde tu baada ya kushuka kutoka kwenye ndege.


Iwapo bunduki moja iliyonaswa nyumbani kwa Rocky itabainika kuwa ndiyo silaha inayotajwa kuhusika na tukio hilo, inaweza kuimarisha kesi kwa waendesha mashtaka ambao bado hawajamfungulia mashtaka Rocky.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad