4/13/2022

"Tangu Aolewe Hakuwa na Amani" Mama Mzazi wa Osinachi Afunguka


Mama na dada wa marehemu Osinachi Nwachukwu (42), wamefunguka kwa mara ya kwanza tangu mwimbaji huyo mahiri wa nyimbo za injili alipofariki siku ya Ijumaa, Aprili 2, 2022.

"Ninaumia kwa ajili ya huyu mkwe wangu, alikuja hapa kutaka kumuoa mwanangu na nikampatia ushirikiano, lakini sasa amechukua uhai wake'' ameeleza Mama mzazi wa Osinachi kwenye mahojiano maalum na Shirika la habari la BBC.

Mama huyo aliongeza kuwa tangu ndoa ya binti yake ifungwe hakuwa na amani, wala Osinachi mwenyewe hakuwa na amani.

Aidha, ripoti za awali zilisema kuwa marehemu Osinachi alikuwa akiugua saratani ya koo, lakini familia yake imekanusha hilo, ikidai kuwa alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.

Hata hivyo, mumewe na Osinachi, Peter Nwachukwu bado hajatoa maoni yake kuhusu shutuma hizo dhidi yake.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger