4/09/2022

Bao la Mayele Sh50 milioniNYOTA wa Yanga wamerudi kambini jana jioni, lakini walipofika tu wamekutana na Sh50 milioni iliyopatikana kupitia bao la kiufundi la straika Fiston Mayele.

Kama uliuangalia vizuri mchezo wa Yanga na Azam juzi, takribani dakika 77 kulikuwa na vita kati ya mabeki wa kati wa Azam wakiongozwa na Aggrey Morris dhidi ya Mayele iliyokuja kuhitimishwa kwa bao hilo la pili lililoipa ushindi Yanga.

Iko hivi. Kama si bao hilo Yanga ilikuwa inapoteza kiasi cha Sh 50 milioni walizoahidiwa na matajiri wao GSM kama posho lakini Yanga iliposhinda tu mambo yakawa uhakika.

Katika mchezo huo Mayele na Aggrey walianza kuonyeshana kazi mapema tu wakionekana kupambana vikali kila mmoja akitafuta ubora wake.


 
Dakika 2, Mayele alipokea krosi ya Saido katika kuunganisha mpira huo ulionekana kuguswa na mkono wa Morris ila mwamuzi wa kati, Nassor Mwinchui hakutafsiri kama penalti na kumwacha straika huyo akilalamika.

Aggrey aliendelea kupambana kumzuia mshambuliaji huyo ambapo dakika ya 6, alimbana alipoingia ndani ya eneo la hatari na kipa wake Ahmed Salula kuuwahi na kuudaka.

Dakika ya 50 na 52 Morris aliendelea kumdhibiti Mayele akitangulia kumzuia kuingia ndani ya eneo la hatari kisha kugeuka na kutoa pasi kwa wenzake.


Kibao kilianza kugeuka dakika ya 66 Mayele aliachia shuti kali Salula akapangua na kudaka tena mshambuliaji huyo akimzidi akili Morris sambamba na Kheri.

Baada ya shambulizi hilo Mayele alimsababishia maumivu Kheri na kulazimika kutibiwa kisha baadaye kushindwa kuendelea na mchezo na kubaki na Morris uwanjani. Dakika ya 78 Aggrey alimsahau kidogo Mayele na kuchoma nyumba.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alisema hatua ya Mayele kubanwa na mabeki hao ilitokana na dosari ya viungo wake wa pembeni Dickson Ambundo na Denis Nkane kushindwa kumsaidia.

“Niliona hiyo hali ya ushindani kwangu mimi ni kitu kizuri kwa kuwa kinamjenga mchezaji lakini ile hali ingepungua kama Ambundo na Nkane wangekuwa wanafanya kazi zao kwa ukaribu kushirikiana na Mayele,” alisema Nabi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger