Ticker

6/recent/ticker-posts

Haji Manara "Mo Dewji Hana Chuki"

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>

 


Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara amesema Rais wa Heshina wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Mohamed Dewji hana chuki na yoyote katika maendeleo ya Soka la Bongo.


Manara ametoa kauli hiyo mapema leo Jumatano (April 27) alipohojiwa kwenye kipindi cha Sports Head Quarter cha Radio EFM, ambapo amesema Mdau huyo mkubwa upande wa Simba Sc amewahi kufanya naye kazi na hakuwahi kuona chuki yake.


Amesema kuna mtu ambaye hakuwa tayari kumtaja, ndio sababu kubwa ya kuingia chuki baina ya watu wa klabu kongwe za soka nchini Tanzania Simba SC na Young Africans SC.


Manara ameongeza kuwa, atakua tayari kumuanika mtu huyo katika mkutano na waandishi wa habari, ambao ameahidi kuufanya baada ya Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22 kufikia ukingoni.


“Namjua Mo Dewji hana chuki, nimekaa nae muda mrefu sana pale Simba SC, lakini kuna mtu ndiyo amekuja kuweka chuki baina ya watu wa Young Africans SC na Simba SC, msimu ukiisha nitafanya Press kubwa kumtaja mtu huyo” amesema Manara


Hata hivyo Manara aliwahi kumsema vibaya Mo Dewji siku chache baada ya kuondoka Simba SC, alipozungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena.


Pia aliwahi kupinga hadharani Cheo cha Rais wa Heshima alichopewa Muwekezaji huyo Mkuu wa klabu ya Simba SC, kupitia Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu hiyo ya Msimbazi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments