4/09/2022KOCHA wa Geita Gold FC, Fred Minziro ameahidi kulipa kisasi dhidi ya Yanga kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), ambao utapigwa Jumapili hii uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Spotileo, Minziro amesema anajua utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora waliokuwa nao Yanga, lakini wamepanga kutumia udhaifu wao, ili kulipa kisasi cha kufungwa mara mbili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

" Ni kweli Yanga timu kubwa na kikosi chao kimeimarika sana msimu huu, lakini tumefuatilia mechi zao nyingi walizocheza hivi karibuni na kuna mapungufu tumeyaona, tumepanga kuyatumia, licha ya uzuri wao lakini wanafungika," amesema Minziro.

Kocha huyo aliyewahi kupita Yanga akiwa mchezaji na kocha, amesema maandalizi yao yanaenda vizuri,  akiamini kesho wataibuka na ushindi.


 
Geita imeanza kucheza Ligi Kuu msimu huu, lakini imeleta ushindani wa hali ya juu kwa timu mbalimbali inazokutana nazo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger