4/10/2022

Museven Aagiza Wanaosema Spika Alipewa Sumu WakamatweRais wa Uganda, Yoweri Museveni ametoa amri kwa Polisi kufuatilia wanaoandika kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah alifariki baada ya kupewa sumu, wakamatwe ili watoe ufafanuzi wa wanachokiandika

Pamoja na kauli hiyo Familia ya Marehemu imeshikilia msimamo wake kuwa Oulanyah ambaye alifariki Machi 19, 2022 akiwa kwenye matibabu Marekani baada ya kutibiwa katika hospitali tofauti nchini #Uganda na Kenya bila mafanikio na alifariki kwa kupewa sumu

Aidha, Naibu Mwenyekiti wa Chama kinachotawala cha National Resistance Movement (NRM), Godfrey Kiwanda amesema Marehemu alimjulisha wakati anaumwa kuwa alipewa sumu muda mfupi baada ya kushinda Uchaguzi wa Spika Mei, 2021


HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger