Musukuma Ajiuzulu Ubalozi Mazingira, Akiikana Ripoti Mto Mara "Magugu Hayawezi ua Samaki"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dodoma. Balozi wa Mazingira anayewakilisha Bunge, Joseph Kasheku (Musukuma) leo Jumanne Aprili 5, 2022 amejiuzulu nafasi hiyo akisema ni aibu kuwa mwakilishi wakati aliyemteua ameunda ripoti ya hovyo.

Musukuma mbunge wa Geita Vijijini amefikia hatua hiyo muda mfupi baada ya tume iliyoundwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Seleman Jafo kuwasilisha kwa wabunge ripoti ya uchunguzi wa chanzo cha kuchafuka kwa maji ya Mto Mara

Ripoti hiyo ni ile iliyofanya uchunguzi wa uchafuzi wa maji kuwa na rangi nyeusi na kusababisha vifo vya samaki katika mto mara ambayo ilikuwa chini ya Profesa Samweli Mayele na wajumbe wengine 10.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Seleman Jafo aliunda kamati kuchunguza chanzo cha tatizo hilo lakini baada ya kuwasilishwa kwa wananchi ilizua mjadala karibu kila kona.


Leo, wabunge 18 wote wameipinga ripoti hiyo na kuomba isiwekwe kwenye mtandao maalumu wa serikali kwa kuwa maelezo yake ni ya aibu.

“Mimi nilikuwa Balozi wa Mazingira ninayewakilisha wabunge ambaye nilichaguliwa na Waziri Jafo (Dk Seleman), natangaza kuanzia leo kuwa nimejiuzuru nafasi hiyo kuanzia leo maana hii ni aibu sana,” amesema Musukuma.

Mbunge huyo amesema hawezi kuingia kwenye mgogoro wa uongo kuhusu tume hiyo ambayo imekuja na majibu yasiyo na uhalisia akisema hata kwa wasiokuwa na elimu wanajua nini kimetokea kwenye mto huo.


Amesema pamoja na Shahada yake ya Udaktari wa lifti, lakini ripoti ya Profesa Manyele inapingana na taarifa kamili za wasomi wenzake hivyo hawezi kuikubali na kuomba iundwe tume nyingine kwa ajili ya kwenda kufanya nyingine yenye uhalisia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad