4/20/2022

Mwigizaji Nguli wa Nigeria Rita Dominic Afunguka Ndoa Akiwa na Miaka 46


Mashabiki wa filamu nchini Nigeria wametumia mitandao ya kijamii kumpongeza msanii wa Nollywood, Rita Dominic, katika siku yake ya harusi.

Picha katika mtandao wa Instagram zinamuonyesha bibi harusi Rita Dominic akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya Kiigbo kabla ya sherehe hiyo.

Baadhi waliandika "Hongera Rita Dominic. Utoto wangu ulikuwa unafuraha nikikuona kwenye televisheni Mungu abariki ndoa yako”

"Upendo wa kweli kamwe hauchelewi”

Dominic, 46, ni mkongwe wa tasnia ya filamu nchini Nigeria na ameigiza katika filamu nyingi maarufu

Harusi hiyo imehudhuriwa na waigizaji wenzake kadhaa wakiwemo Joke Silva, Uche Jombo, Kate Henshaw na Ini Edo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger