4/19/2022

Mwimbaji wa nyimbo za injili toka Kenya, Ringtone Apoko Alikashifu Tamasha la Nyashinski


Mwimbaji wa nyimbo za injili toka Kenya, Ringtone Apoko amekashifu tamasha aliloandaa mwanamuziki Nyashinski katika uwanja wa Carnivore huko Nairobi, akisema ulikuwa mkutano wa uzinzi.

Ringtone kupitia ukurasa wake wa Instagram, ame-share video ambayo inamuonyesha akitumbuiza mbele ya watoto na kwenye maelezo yake akaandika, “Tumejitolea kuwekeza katika vizazi vijavyo na Nyashinski anang’ang’ana kusaidia watu kuzini. Aibu kwako kwa tamasha lililojawa mapepo huko Carnivore.”

Tamasha la Nyashinski lililoitwa “Shin City” liliandaliwa usiku wa Jumamosi, Aprili 16 mwaka huu katika uwanja wa Carnivore jijini Nairobi.

Kabla ya kuanza kwa tamasha hilo, Nyashiski alitangaza kwamba tiketi zilikuwa zimeuzwa zote. Tamasha la Shin City lilipewa nguvu na kampuni ya kutengeneza pombe ya Kenya Breweries Limited (KBL), kupitia vinywaji vya Tusker na Johnnie Walker.

SNS

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger