TANESCO wanafanya tathmini Bwawa la Nyerere

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Shirika la umeme nchini Tanesco, limesema linafanya Tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao ujenzi wake umefikia asilimia 58.84 ukitarajia kukamilika mwaka 2024.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau wa maendeleo wakiwemo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Maharage Chande amesema hivi sasa wanafanya tathmini ya kazi iliyofanyika na kuangazia changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

Awali, Mkurugenzi huyo alielezea kuanzishwa kwa mfumo wa ‘Nikonekt’ ambao ni maalumu kwa wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme kidigitali. Application hii inafanya mteja kutokuwa na haja ya kwenda kutafuta kishoka ili apate umeme, kama mteja anatumia kitochi, laptop, au smartphone ataweza kupata huduma hii, aliongeza kwa kusema itapunguza maswala na rushwa na watanzania wengi wanaenda kufurahia huduma ya haraka kutoka Tanesco.

Kupitia programu hii management ya Tanesco itaweza kuona utendaji wa kazi pamoja na utoaji huduma.


 
Naibu Mkurugenzi wa usambazaji na huduma kwa wateja Mhandisi Athanasius Nangali, alielezea mfumo unaotumika hivi sasa wa kusikiliza kero za wateja na kuzitafutia ufumbuzi. Pia imezungumza na baadhi ya wadau wa maendeleo juu ya matumizi ya mifumo ya teknolojia katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad