4/12/2022

Treni ya umeme kutoka Dar es Salaam -Morogoro kujaribiwaMKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, treni inayotumia umeme itatoka Dar es Salaam hadi Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hiyo ni baada ya miundombinu ya umeme katika kipande hicho kukamilika kwa asilimia 100.

Akizungumza leo Jumanne Tarehe 12 Aprili, 2022 katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa kipande cha Makutupora—Tabora (kilomita 368), Kadogosa amesema, “katika historia ya Tanzania treni inayotumia umeme itatoka Dar es Salaam hadi Morogoro wiki mbili zijazo.”

Amesema Jumapili iliyopita walifanya safari ya kwanza kutoka kituo cha Dar es Salaam hadi Morogoro, “kwa maana nyingine ni kwamba tumeshaunganisha reli na utandikaji reli umeshaisha kuanza Dar es Salaam hadi Morogoro.”

“Tunategemea wiki ya mwisho ya mwezi huu kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania treni ya umeme itapita kuanzia kituo cha Dar es Salaam mpaka Morogoro,” amesema Kadogosa.

Amesema kipande hicho kimeshakamilika kwa asilimia 95.32 na kazi iliyobaki ni kuinganisha na bandari ya Dar es Salaam pamoja na kukamilisha njia za watu na magari Vingunguti na Uwanja wa Mwalimu Nyerere na njia ya kwenda Banana.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger