4/17/2022

Uchunguzi Tuhuma za Kingono kwa Mnigeria Hotelini Zanzibar WaanzaTume ya Utalii Zanzibar, imeshtushwa na taarifa ya mwanamke kutoka nchini Nigeria, Zainab Oladehinde, anayedai kutaka kuingiliwa kingono na mtu asiyemfahamu akiwa ndani ya chumba cha hoteli aliyofikia visiwani humo, na kusema kwamba uchunguzi wa madai hayo umeanza.
Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke huyo kuandika waraka wa tuhuma hizo kupitia mtandao wake wa Twitter, akituhumu kufanyiwa kitendo hicho mnamo mwezi Aprili 2021, alipofika visiwani humo kwa ajili ya mapumziko yake ya kusherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa.

Zainab anadai kwamba mwanaume huyo hakufanikiwa kumwingilia kimwili baada ya kumwambia kuwa ni vyema akatumia kondomu kwani yeye ni mwathirika wa VVU na ndipo mwanaume huyo alipoondoka chumbani humo akiahidi kwenda kuchukua kinga hizo.

Zainab ameendelea kudai kwamba, hata alipojaribu kuhitaji msaada wa hoteli hiyo hakupata ushirikiano mzuri jambo ambalo anadai pia hata alipokwenda polisi hakupata msaada stahiki.

Tume ya Utalii Zanzibar, imeeleza kwamba huo sio ukarimu wa Wazanzibari na kitendo hicho si cha kiungwana kwa mtalii yeyote.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger