Ticker

6/recent/ticker-posts

Urusi yadai kushambulia ngome 315 za Ukraine usiku kucha

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAVyombo vya habari vya serikali ya Urusi vinaripoti kuwa jeshi lake lilishambulia jumla ya malengo 315 nchini Ukraine usiku kucha na miji kadhaa ikishambuliwa Jumatatu.

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa imeharibu maghala manne ya silaha na vifaa vya kijeshi nchini Ukraine usiku kucha kwa makombora ya Iskander, kombora la masafa mafupi, shirika la habari la TASS linaripoti.

"Makombora ya anga ya juu yaliharibu vituo 16 vya kijeshi vya Ukraine usiku wa kuamkia leo," msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov alisema.

Aliongeza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi iliwaangusha wapiganaji wawili wa Ukraine.


 
BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai haya.

Hata hivyo Yuri Sak - mmoja wa washauri wa waziri wa ulinzi wa Ukraine, ambaye yuko magharibi mwa Ukraine - amekuwa akizungumza na BBC kuhusu mashambulio katika mji wa Lviv.

"Kilichotokea leo ni kitu cha kutisha kwa sababu hili ni shambulio kubwa la kombora [dhidi] ya miundombinu ya kiraia," aliambia kipindi cha Leo cha BBC Radio 4.

Post a Comment

0 Comments