4/23/2022

Watetezi haki za binadamu wafungua kesi ya dhamana kwa Madeleka

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), wamefungua kesi ya kuomba dhamana ya Wakili Peter Madeleka, aliyekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, tarehe 20 Aprili 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na THRDC, kesi hiyo Na. 16/2022, imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo imefunguliwa na THRDC pamoja na LHRC, kupitia Mawakili, Mpale Kaba Mpoki, Jebra Kambole, Hassan Ruhanywa na Paul Kisabo, dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Washtakiwa wengine ni, Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IGP) na Afisa wa Makosa ya Jinai Kanda ya Dar es Salaam.


 
“THRDC kwa kushirikiana na LHRC wakiongozwa na mawakili wamefungua kesi ya kuomba dhamana mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kesi imepangwa kusikilizwa Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2022, saa sita kamili mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi Kyaruzi,” imesema taarifa ya THRDC.

Madeleka alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa katika maeneo ya maegesho ya magari ya Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Mtandao huu ulimtafuta Wakili Kisabo, kwa njia ya simu leo Jumamosi, tarehe 23 Aprili 2022, kujua makosa anayotuhumiwa Wakili Madeleka, ambaye amesema hadi sasa haijulikana tuhuma zake.


“Hawajasema wanamshikilia kwa makosa gani , mimi wameninyima access ya kumuona. Sina taarifa kama amehojiwa au hajahojiwa, ningepewa taarifa ningejua amehojiwa kwa makosa gani,” amesema Wakili Kisabo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger