4/24/2022

Watu 9 Waliopotea Katika Boti ya Japan Wakutwa Bila ya ufahamu


Watu 10 kati ya 26 ambao walikuwa katika boti ya kitalii ambayo iliyotoweka jana huko Japan wamepatikana leo katika pwani ya kaskazini taifa hilo wakiwa wamekufa. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa walinzi wa fukwe.

Likinukuu chanzo hicho shirika la habari la Uingereza Reuters awali kilisema, watu hao miongoni mwa wengine walikuwa wakijivinjari katika kisiwa cha Hokkaido walikutwa hoi pasipo kujitambua.


Mamlaka nchini Japan zipo katika jitihada za uokozi kwa kutumia ndege, boti za doria, zikijumuisha meli saba, ndege tatu na helkopta nne za walinzi wa pwani, kuisaka boti ya abiria ya "Kazu 1" iliyokumbwa na dharuba katika rasi ya Shiretoko jana Jumamosi

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger