Waziri Aweso Ageuka Mbogo, Milioni 600 za Bwawa ziko Wapi ? Nionyesheni Lilo Bwawa la Milioni 600

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri Aweso achukizwa na matumizi mabaya ya Ml.600 za mradi wa maji Handeni; Achukua hatua kali.


Zaidi shilingi milioni 600 zatumika vibaya Wilayani handeni Mkoani Tanga, Fedha hizo zilizotengwa kwa ajali ya kukamilisha mradi wa bwawa la maji la kata ya Kwemkambala ambapo mradi huo mpaka sasa umeshindwa kutekelezeka

Hatua hiyo imemchukiza Waziri wa maji Jumaa Aweso baada ya kulalamikiwa na wananchi na wahusika kushindwa kumpa maelezo sahihi ya matumizi ya fedha hizo .

Aidha waziri huyo amewachukulia hatua waliohusika na ubadhilifu wa fedha hizo ambao ni mtaalamu wa mabwawa kutoka wizara ya maji, mthibiti ubora wa wizara hiyo pamoja na Mkandarasi wa mradi huo .


“Serikali inayoongozwa na Rais samia haiwezi kuvumilia uzembe wa aina hii mnasema fedha zimetumika kumlipa mkandarasi na hapa hakuna kazi inayoonekana ocd wachukue hao wakatoe maelezo sahihi” Alibainisha wazir Aweso.

Waziri amesema fedha hizo zilipelekwa mahususi kwa wananchi wa eneo hilo waweze kupata maji safi na kuwaondolea adha hiyo ambayo inawabili tokea mwaka 2018 .

Awali akitoa malalamiko mbele ya Waziri diwani wa Kwedihamba Musa Abedi amesema wananchi wa eneo hilo walipisha mradi huo tokea mwaka 2019 mpaka leo hawapata maji na mashamba yao yalichukuliwa.


Kama mkandarasi anaweza akalipwa Fedha zaidi ya milioni 300 na hajafanya chochote mpaka leo wananchi hawana maji kwanini wasilipwe fidia maana wengine walikuwa na mashamba yao eneo hilo”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad