4/25/2022

Yericko Nyerere Aishauri Simba SC Baada ya Mchezo wao na Orlando Pirates

 


Mwanachama na Shabiki Kindakindaki wa Simba SC Yericko Nyerere ameonesha kuridhishwa na uwezo wa kikosi cha Simba SC kilichopambana dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini leo Jumapili (April 24).


Simba SC imecheza ugenini Afrika Kusini na kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa changamoto ya Penati 4-3, baada ya wenyeji wao kupata bao ambalo liliufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1

Simba SC ilishinda 1-0 jijini Dar es salaam Jumapili (April 17).

Yericko ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook na kumshukuru kila mmoja ndani ya Simba SC kwa kuzingatia nafasi yake, huku akitoa ushauri wa kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao kwa ajili ya michuano ya CAF na Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Yericko ameandika: Mpira umeisha, @simbasctanzania tumetolewa, Vijana wetu wamecheza kwa nguvu zote na kwahakika tunajivunia wao. Tujipange michuano mingine ya Klabu Bingwa mwakani, Tunahitaji kusajiri washambuliaji wenye sifa ya michua ya CAF.

Lazima pesa iwekwe sio maneno, Tunamhitaji @victorien_adebayor_ na @moses.phiri na ikimpendeza kocha basi na @aziz_ki_stephanie10. Timu yetu ukiiangalia inapocheza bila hata kuwa na taaluma ya mpira unaona kwamba tunakosa mshambuliaji wa kati zaidi.

Congratulations sana Simba, Mashabiki, Uongozi wote na wachezaji, Pongezi kubwa kwa Mdhamini @moodewji na mtendaji mkuu Bi @bvrbvra kazi kubwa ya kuongoza taasisi kubwa kama simba inahitaji mwanamke wa shoka kwelikweli. Na mwisho pongezi kubwa kwa @ahmedally_ kwa maheuzi makubwa ya idara ya habari ya klabu yetu.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger