5/29/2022

Ahmed Ally "Hatuna namna tujipange msimu ujao"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Meneja wa mawasiliano Simb SC, Ahmed Ally amesema kuwa watayafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza msimu huu ikiwemo kukiboresha kikosi chao.

”Hatuna namna tujipange kwaajili ya msimu ujao, kitu ninachoweza kuwaahidi wanasimba ni kwamba tumeshaona ni wapi kwenye mapungufu, wapi panamatatizo tuna waahidi kwamba tunakwenda kufnya maboresho makubwa ndani ya timu yetu, tunakwenda kufanya usajili mkubwa wa timu yetu ili kuhakikisha kwamba msimu ujao hatupitii mateso tunayopitia msimu huu.”

Simba SC msimu huu imeshindwa kutimiza hata lengo moja kati ya yale matatu waliyojiwekea mbele ya Kocha Pablo, ikiwemo kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho, kuchukua kombe la Azam Sports Federation Cup pamoja na Ligi Kuu.

Hata hivyo Simba imeonekana kutofurukuta anapokutana na mtani wake Yanga SC msimu huu ikiwemo kupoteza Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup na Ngao ya Jamii.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger