DPP asubiri jalada kuachiwa Sabaya

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
MKURUGENZI Mkuu wa Mashitaka Nchini (DPP), Sylivester Mwakitalu, amesema anasubiri jalada la kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha lenye uamuzi wa rufaa ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (35) na wenzake wawili.

Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma aliyeteuliwa kuisikiliza rufaa hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Ijumaa aliwachia huru Sabaya, ambaye alikuwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo na wenzake wawili.

Walioachiwa ni Sylivester Nyengu (26) mshitakiwa wa pili na Daniel Mbura (38) mshitakiwa wa tatu, kwa sababu baadhi ya mashahidi katika kesi hiyo hawakuhojiwa maswali ya dodoso na mawakili wa wakata rufaa, hatua ambayo alisema ni kuwanyima haki ya msingi watuhumiwa hao.

Akizungumza na Habarileo mjini Arusha leo, mara baada ya mapumziko mafupi ya mafunzo ya mawakili wa serikali na Waendesha Mashishitaka wa Serikali yanayofanyika jijini hapa, DPP amesema jalada la kesi ya Sabaya bado halijamfikia ofisini kwake.


 
Lakini amesema likimfikia atakaa na timu ya wataalamu wake na kuchambua kipengele kimoja baada ya kingine na baada ya hapo atajua la kufanya.

‘’Ninasubiri jalada la kesi ya Sabaya ofisini kwangu na likija nitatoa taarifa rasmi, baada ya kukaa na wataalamu wangu kuiangalia na kuusoma uamuzi wa Jaji, kama tunakata rufaa ama la, lakini kwa sasa siwezi kusema chochote,’’amesema Mkurugenzi wa Mashitaka

Sabaya, Nyengu na Mbura Oktoba mwaka jana, walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja, baada ya kukutwa na hatia ya kuteka, kupora na kuiba kwa kutumia silaha kiasi cha Sh milioni  2.7 katika duka la Shahiid Store la mjini Arusha.


 Lakini Ijumaa Mei 6, 2022 Jaji Kisanya aliwaachia huru, ingawa Sabaya na Nyengu walirudi rumande kusubiri hukumu yao ya kesi ya uhujumu uchumi inayotarajiwa kusomwa Mei 31 mwaka huu. Mshitakiwa wa tatu Mbura yeye aliachiwa kurejea nyumbani kwani hana kesi nyingine.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad