Haji Manara atuhumiwa kudanganya Kuhusu Mashabiki Waliohudhuria Simba na YangaBaadhi ya Wadau wa soka la Tanzania wamemshambulia Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara kufuatia picha aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, inayoonyesha mashabiki wa klabu hiyo wakiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Manara amedai kuwa Mashabiki wanaoonekana kwenye picha hiyo ni wale walioingia Uwanja wa Benjamin Mkapa Jana Jumamosi (April 30), kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC, huku Young Africans ikiwa mwenyeji.

Asilimia kubwa ya wadau waliotoa maoni yao kwenye picha hiyo, wamedai kuwa Manara amedanganya kwa kuweka picha ya Mashabiki wa Young Africans waliohudhuria kwenye Tamasha la Mwananchi (Siku ya Mwananchi) 2021, ambapo klabu hiyo ya Jangwani ilicheza dhidi ya Zanaco FC na kupoteza kwa mabao 2-1.

Katika picha hiyo Manara ameandika ujumbe unaosomeka: Asanteni Wananchi, takwimu zimeonyesha over two third ya washabiki jana mlikuwa nyie. ( THELUTHI MBILI)


Hii ni heshma kwetu na lengo letu mlilitimiza kwa kiwango kikubwa.

Isingejaa wangesema ni kwa sababu hawajatumia Vispika vyao kuuzia sumu za kuulia kuku mdondo na kunguni pori, mechi imejaa wanasema ni kawaida ya game hz kujaa, halaf na Pua wanabana kabisa bila haya 🤪🤪

Samaki hafundishwi kupiga Mbizi ni kawaida yake.


Wananchi eeeeh, hili la ubingwa tusibweteke nalo bado.

IS NOT OVER, UNTIL IS OVER

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad