Kumekucha..George Mpole Amuacha Mayele Akishangaa Mataa, Geita Gold ikipaa Tatu Bora

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mpole anashika rasmi usukani kwa mabao 13 dhidi ya Mayele (12) na kuifanya Geita Gold kuwa nafasi ya tatu kwa alama 34, huku Mbeya Kwanza hali ikizidi kuwa tete kwenye vita ya kukwepa kushuka daraja.
mpole pic
Mbeya. Bao alilofunga Straika George Mpole limemfanya kuongoza katika orodha ya wafungaji Ligi Kuu akimuacha mpinzani wake, nyota wa Yanga Fiston Mayele.

Leo akiiongoza Geita Gold dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo uliopigwa uwanja wa Majimaji mjini Songea, Mpole alitumia dakika 11 tu kuwaua wapinzani hao na kumuongezea Mayele presha zaidi ambaye amecheza mechi tatu mfululizo bila 'kutetema'.

Mpole alifunga bao hilo baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa wapinzani wao na mpira kumkuta mfungaji huyo eneo sahihi na kukunjua shuti lililomshinda Kipa Hamad Kadedi.

Hata hivyo Mbeya Kwanza walipambana kusawazisha lakini mabeki wa Geita Gold walikuwa imara kudhibiti hatari zote zilizolenga lao lao na kufanya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa wenyeji kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa 1-0.


Kipindi cha pili wenyeji ndio walianza kufanya mabadiliko, ambapo Eliuta Mpepo na Issa Kanduru waliwapisha Oscar Mwajanga na Edgar William dakika ya 56 huku Geita wakiwatoa Raymond Masota na kumwingiza Hassan Ramadhan dakika ya 63 na Edmund John kumpisha Juma Mahadhi dakika ya 84

Hata hivyo Mbeya Kwanza walipata pigo kwa kucheza pungufu baada ya Straika wake, Enock Jiah kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kadi mbili za njano dakika ya 74 na kuwafanya vibonde wao kumaliza dakika takribani 15 za mwisho wakiwa pungufu.

Kwa matokeo hayo, Mbeya Kwanza wanabaki mkiani kwa pointi 23 na kuendelea kuwa kwenye wakati mgumu wa kukwepa kushuka daraja, huku Geita Gold wakichumpa hadi nafasi ya tatu kwa alama 34.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad