Ticker

6/recent/ticker-posts

Kajala Kurudiana na Harmonize ni Maamuzi yake Watu Itabidi Tumuelewe na Tukubali


Kajala amerudiana na @harmonize_tz

Kajala hawezi kurudiana na @harmonize_tz

Kajala itakuwa aibu kurudiana na mtu ambaye alimtaka mtoto wake @therealpaulahkajala

@kajalafrida atakuwa amefata furaha yake ya kweli akirudiana na @harmonize_tz

HII YOTE NI MIJADALA AMBAYO MSINGI WAKE NI MAWAZO NA MAONO YA @kajalafrida

Kifupi ni kwamba katika maamuzi yoyote ambayo @kajalafrida ataamua kufanya juu ya mahusiano yake na @harmonize_tz iwe kurudiana au kutorudiana basi itabidi watu tu wamuelewe Kwa sababu kila kitu kilichotokea nyuma ni matokeo ya malezi yake.

Ikiwa KAJALA anarudi Kwa HARMONIZE ni sawaa kabisa sababu yeye ndio mzazi wa @therealpaulahkajala na yeye ndio alikuwa anajua uchungu wa kuona mwanaume ambaye unalala naye uchi akawa anatamani kulala na mtoto wako Kama ambavyo analala na wewe.

Sasa kama anaamua kusema Leo nasamehe na nasema Ile ilikuwa kazi ya shetani ana haki ya msingi kabisa na inabidi watu waheshimu sababu mwisho wa siku yeye ndio anajua mazingira gani alitengeneza Kwa mtoto wake mpaka kufika walipofika.

Lakini kama @kajalafrida anasema siwezi kumsamehe mtu ambaye alitaka ku share mapenzi na Mwanangu wa kumzaa inabidi aheshimiwe sababu yeye ndio mzazi na yeye ndio anajua uchungu wa kuona mwanaume uliyelala naye anataka pia kulala na mtoto wako wa kumzaa.

Lakini mwisho wa siku hayo yanabaki kuwa maamuzi ya @kajalafrida ambaye mtoto kamzaa mwenyewe na furaha anaitafuta mwenyewe na maisha ni yake mwenyewe hakuna wa kumpangi mfumo wa maisha yake sababu toka mwanzo alishajua matokeo ya kile alichokipandikiza.

Kwenye maisha Kuna wakati unafika ukitaka kufanya maamuzi basii huwa hutakiwi kusikiliza watu bali unasikiliza Ile sauti ambayo inatoka ndani ya moyo wako hiyo ndio yenye umuhimu zaidi kwenye nyakati ambazo unatakiwa kufanya maamuzi magumu ambayo unajua kabisa Kuna watu watafurahi na Kuna watu watakwazika.

FURAHA NI YAKE NA MTOTO NI WA KWAKE PIA.

By Abby

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments