Mbunge Msukuma "Spika Sinta Piga Sarakasi Ila Naomba Niimbe Bungeni"


Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson amesema ni marufuku kuimba ndani ya Bunge kama ilivyo kupiga magoti au sarakasi ambapo ameyasema haya baada ya Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma kutaka kuimba ili kumpongeza Rais Samia wakati wa mjadala wa azimio la kumpongeza Rais Samia kwa kutajwa miongoni mwa Viongozi wenye ushawishi mkubwa duniani na pia kupewa tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu.

Hoja ya Azimio hilo la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan imewasilishwa Bungeni Dodoma leo na Mbunge wa viti Maalumu Zainabu Katimba.

Rais Samia Suluhu Hassan alipewa tuzo hiyo ya Mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye kama mchango wa kutambua mafanikio ya Serikali ya Awamu ya sita katika Ujenzi wa Miundombinu ya usafirishaji ambayo kwa kawaida hutolewa kwa mkuu wa nchi iliyofanya vizuri katika sekta hiyo na pia ametajwa kuwa miongoni mwa Viongozi mia moja wenye ushawishi mkubwa duniani kwenye Jarida la TIME la May 24 2022.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad