5/20/2022

Muliro Azungumzia Tukio la Mwanamke Mkazi wa Sinza Aliyejeruhiwa kwa Risasi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAKAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amethibitisha tukio la Mwanamke aitwaye Mariam mkazi wa Sinza Lion Dar es Salaam kujeruhiwa kwa risasi majira ya saa 12:00 asubuhi ya leo Mei 20, 2022 maeneo ya Sinza Lion, na kusema imempata kwa bahati mbaya baada ya Askari kufyatua risasi juu kwa lengo la kuwatawanya wananchi waliokuwa wanampiga mwizi wa simu.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo wakati akizungumza, ili kutoa ufafanuzi wa madai yaliyotolewa na mashuhuda wa tukio hilo kwa kusema kwamba mwanamke huyo aitwaye Mariam amejeruhiwa na polisi.

 

“Ni kweli tukio hilo limetokea na jeshi linaendelea kulifuatilia, lakini ni kwamba askari walifyatua risasi juu katika juhudi za kumuokoa mtuhumiwa na kwa bahati mbaya kuna mwanamke amejeruhiwa ingawa anaendelea vizuri,” amesema Kamanda Muliro.

 

Aidha Kamanda Muliro akimzungumzia mwizi huyo amesema, “Huyo mtuhumiwa hatujamtambua kwa sababu hajaweza kuongea, alikuwa tayari amepigwa, hawezi kuongea, hivyo tunalichunguza tukio hilo”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger