6/09/2022

Aliyeiba Kanisani Aomba Kutubu kwa Mchungaji Kabla ya Kupelekwa Jela

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAJohn Kiiru, Mtuhumiwa
KIJANA mmoja aliyebainika kuiba vifaa vya muziki kwenye kanisa la Kenya Assemblies of God (KAG) mjini Eldoret nchini Kenya ameomba mahakama imruhusu akatubu.

John Kiiru mwenye umri wa miaka 18 aliyekiri kuiba vitu hivyo aliitaka

mahakama kumruhusu kuomba msamaha kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo kabla ya kufungwa jela akidai pia kuwa anataka kukombolewa kabla ya kwenda jela.

Mshukiwa alimwambia hakimu wa mahakama ya Eldoret, Dennis Mikoyan, kuwa anataka kutumia kifungo chake gerezani kuwahubiria wafungwa wengine baada ya kugeuzwa kuwa ‘Kuzaliwa kwa mara ya pili katika Kristo’.

“Nimejutia sana nilichofanya, naomba mahakama hii inisaidie kumfikia pasta wa kanisa na viongozi wengine kuomba msamaha kabla ya kuhukumiwa,” aliiambia mahakama wakati akihukumiwa.

Hukumu ya kesi hiyo iliyovuta hisia ya watu wengi nchini humo inatarajiwa kutolewa mahakamani mnamo Juni 27, 2022.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger