6/23/2022

John Mnyika "Hakuna Sababu Akina Halima kuwa Bungeni"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kesi ya msingi iliyokuwa imefunguliwa na wabunge 19 akiwemo Halima Mdee, waliovuliwa uanachama na chama cha CHADEMA hivyo kuruhusu taratibu zingine kuendelea.


Akizungumza na vyombo vya habari mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakili wa CHADEMA Peter Kibatala, amefafanua kuwa Mahakama pia imetupilia mbali maombi ya msingi ya kutaka kupewa kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama.


Aidha Kibatala ameeleza kuwa miongoni mwa sababu ya kutupiliwa mbali kwa maombi hayo ni kukosewa kwa jina la mjibu maombi namba moja ambaye ni Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA iliyosajiliwa.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameomba sasa sheria kufuata mkondo wake, akibainisha kwa sasa hawaoni sababu ya wabunge hao kuendelea kusalia bungen

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger