Ticker

6/recent/ticker-posts

Manara Kaamka na Hili Kuhusu Sure Boy..Adai Akizembea Imekula Kwake na Huenda Isijirudie Tena

 


Yanga wamebeba Ubingwa wa Ligi Kuu Bara 2021/2022 pasipo kupoteza mchezo wowote mpaka sasa huku wakiwa wamecheza michezo 29, wakishinda michezo 21 na kusuluhu michezo 7.

Yanga hawajapoteza mchezo mpaka sasa, na mchezo wao wa mwisho wanacheza leo katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar.


Sasa Afisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kwamba lengo lao ni kumaliza msimu huu pasipo kupoteza mchezo licha kuwa tayari wameshachukua Ubingwa.


Katika kulisisitiza hilo Manara amemwambia mchezaji nyota wa eneo la Kiungo wa Kikosi cha Yanga, Abubakar Salum 'Sure boy' kuichukulia kwa uzito mechi ya leo kwani itaandika historia kwake.


Iwapo Sure boy hatopoteza mechi ya leo basi atakua mchezaji wa kwanza Yanga kubeba ubingwa na timu mbili tofauti pasipo kupoteza mchezo.


Sure Boy alibeba Ubingwa na Azam msimu wa 2013/2014 pasipo kupoteza mchezo wa Ligi kwa hivyo ni rekodi ambayo atakuwa amejiwekea kama mmoja wa wachezaji wachache waliofanikiwa kufanya hivyo.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments