6/18/2022

Mayele Amtupia Kombora Mpole, Adai Kila Mtu Ashinde Mechi Zake

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


KINARA wa mabao wa Ligi Kuu Bara, Mkongomani Fiston Mayele ameibuka na kumwambia mpinzani wake wa Geita Gold, George Mpole hatakubali akiache kiatu cha ufungaji bora msimu huu.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya juzi kufunga mabao mawili na kufikisha mabao 16 katika ufungaji huku mpinzani wake akifunga 15.

Mkongomani huyo alifunga mabao hayo katika mchezo wa ligi waliocheza juzi dhidi ya Coastal Union ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na kumalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-0.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mayele alisema kuwa anaheshimu kiwango bora cha Mpole ambacho kinamfanya yeye aongeze juhudi ya kuendelea kufunga.

Mshambuliaji wa Geita Gold FC na Timu ya Taifa ya Tanzania George Mpole

Mayele alisema kuwa licha ya kiwango bora alichonacho Mpole, hamhofii na badala yake ataendelea kupambana uwanjani ili kuhakikisha anamzidi kwa mabao.

“Mimi na Mpole kila mmoja anaipambania timu yake ipate ushindi kwa kutumia vema kila nafasi anayoipata katika kufunga mabao.

“Awali kasi yangu ya kufunga mabao ilipungua kutokana na presha iliyokuwepo ya ubingwa, lakini baada ya kujihakikishia nafasi ya ubingwa wa ligi, nitacheza kwa utulivu ili kufanikisha malengo yetu.

“Haitakuwa rahisi kwangu kuchukua ubingwa, bila ya kupambana kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kufanikisha malengo yetu,” alisema Mayele.

Na Wilbert Molandi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger