6/10/2022

Mungu Tusaidie Watu 18 Wafa Ajali ya Basi Mafinga

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Iringa. Watu 18 wamefariki dunia papo hapo baada ya basi dogo aina ya Costa kugongana uso kwa uso na lori la mizigo karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkiani Iringa.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Juni 10, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea vifo hivyo akisema kuwa taarifa ziaidi zitatolewa baadaye

"Ni kweli ajali imetokea na inasadikika watu zaidi 10 wamepoteza maisha papo hapo," amesema.

Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya watu walio katika eneo la tukio wamesema mpaka saa tatu asubuhi, jitihada za kuokoa majeruhi na kutoa miili ya watu zinaendelea.


Eneo ambalo ajali hiyo imetokea, ndilo ambalo basi la Majinja liliangukiwa na lori mwaka 2015 na kuua zaidi ya watu 40.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger