6/22/2022

Mwanafunzi Agongwa na Basi la Shule Afariki

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


MWANAFUNZI wa darasa la awali Shule ya Msingi Samuu iliyo katika manispaa ya Shinyanga, Godlight Chisawilo (4) amefariki dunia kwa kugongwa na basi la shule hiyo, baada ya kumaliza kumshusha nyumbani kwao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando amesema tukio hilo limetokea jana saa 12 jioni.

Alisema dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T.151 DAG Kassim Mahona (40), alikuwa akimshusha mwanafunzi huyo nyumbani kwao mtaa wa Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga, na alipokuwa akigeuza basi hilo hakumwona mtoto huyo ndipo akamgonga.

“Dereva wa basi hili tunamshikilia kwa ajili ya kujibu mashitaka yanayomkabili ya kumgonga Mwanafunzi na kusababisha kifo chake,” alisema Kayando.

“Chanzo cha ajali hii ni uzembe wa dereva kwa kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara,” aliongeza.


Aidha, alitoa wito kwa madereva wote wa vyombo vya moto mkoani humo kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kutosababisha ajali zisizo za lazima zitokanazo na uzembe.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger