6/04/2022

Rayvanny Afunguka Adai Nyumba Aliyoichoma Ilikuwa Nyumba ya Mchongo

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


RAYVANNY au Vanny Boy; ni staa mwingine mkubwa wa muziki nchini Tanzania ambaye amewafanya watu kuzungumza kwenye mitandao tofauti ya kijamii.

Hii ni baada ya kusema sababu iliyomfanya kuchoma nyumba yake saa chache baada ya kuijenga.
Kwa mujibu wa Rayvanny, alichoma nyumba wakati wa upigaji picha za video kwa ajili ya ubunifu tu, jambo ambalo limezua tafrani mtandaoni.


Nyumba iliyochomwa na Rayvanny kwa ajili ya kuandaa video
Kumbuka Rayvanny si mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika Mashariki ambaye anatumia pesa nyingi kwa ajili ya ubunifu katika video.

Kuna msanii kama Diamond Platnumuz, King Kiba, Harmonize, Zuchu, Nandy na wengine ambao wanatumia pesa nyingi kwa ajili ya ubunifu.


Rayvanny amesema amechoma nyumba kwa ajili ya kuongeza ubunifu
Sasa habari hii kuhusu Rayvanny kuchoma nyumba kwa ajili ya ubunifu imeenea mtandaoni ambapo inazua hisia tofauti kwa sasa.


Wengi wanadai kuwa Rayvanny anaiga kutoka kwa wanamuziki wa kimataifa huku wengine wakijiuliza inakuwaje mtu ajenge nyumba na kuichoma kwa wakati mmoja wakati mwenyewe anaishi kwenye nyumba ya kupanga?
Hata hivyo, wajuzi wa mambo hayo wanasema haikuwa nyumba ya ukweli bali ilikuwa ni pambo la nyumba huku wengi wakisema ilikuwa nyumba ya maboksi au ya mchongo.
Kwa mujibu wa Rayvanny hiyo ni mojawapo ya video ambazo ametumia pesa nyingi kwa sababu ya ubunifu.

Sifaelpaul
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger