6/08/2022

Simba Waanza Kusuka Upya Kikosi, Wengi Kupewa Mkono wa Kwaheri

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Simba kusuka upya kikosi
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema tayari wameanza mchakato wa kukisuka upya kikosi chao kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao.

Akizungumza na Spotileo, kiongozi huyo amesema kufanya vibaya msimu huu kumewashtua na sasa wamepanga mipango mkakati kuhakikisha msimu ujao wanarudi kwa nguvu kubwa.

“Mashabiki wasiwe na hofu kufanya vibaya kwa Simba, sote imetuuma kitu cha msingi ambacho tumeamua kukifanya kwa haraka ni kuanza mchakato wa kukisuka upya kikosi chetu ili msimu unaokuja tuweze kurudi kwenye ubora wetu, “ amesema Try Again.

Amesema mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii tayari watakuwa wameshakamilisha usajili wa nyota kadhaa wakigeni ambao wanaamini watachangia kuirudisha Simba kwenye ushindani kama ilivyokuwa misimu iliyopita.


Simba msimu huu imepokwa mataji yote mawili iliyokuwa ikiyashikilia na mtani wake Yanga ambayo huenda ikayahamishia Jangwani kutokana na timu hiyo kuwa katika nafasi nzuri kwenye michuano yote ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger