6/08/2022

Wakazi Amshukia Babu Tale " Sio Sawa Kumdogosha Lulu DIVA Kisa Unamtetea Msanii Wako, Jitihada za Lulu Zinaonekana"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Rappa Wakazi ametia neno baada Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale maarufu Babu Tale kuhoji kuhusu mirabaha wanayopewa wasanii na Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA).


Itakumbukwa, akiwa Bungeni Babu Tale alisema; Mimi nina msanii wangu anaitwa Kassim Mganga, hakuna asiyeimba nyimbo zake kwenye msimu wa harusi. Kassim Mganga unamuita unampa Mrabaha Sh50,000 halafu unamuita Lulu Diva unampa Sh550,000, umetumia vigezo gani? alihoji Babu Tale.


Wakazi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; "Intentions may be good, but approach not so much. TUPAMBANIE KIWANDA NA SIO MSANII MMOJA MMOJA.


Ni muhimu KUHOJI, ila vizuri zaidi KUSHIRIKI kwenye KUTATUA kwa kutoa MAPENDEKEZO ya kipi kifanyike. Ila Vibaya zaidi hapa Babu Tale amedogosha jitihada za Mtoto wa Kike Lulu Diva ili tu kutetea msanii wake Kassim Mganga (GWIJI).


SIO SAWA Nimeona kipande cha hoja za MwanaFA, amehoji vizuri kuhusu Numbers, na kupitia hapo zipo njia ambayo zinaweza kutumika na Wizara, Cosota, etc kuboresha. Ila tusilete mambo ya mazoea alafu tukadogosha ambao tunawachukulia poa. Mimi binafsi ninaheshimu anachofanya Lulu, jitihada zake hazijifichi.


Viongozi tupambane ili kila mtu apate zaidi na sio kuona mwingine hastaili anachopata tena Binti, ambaye haihitaji hata maelezo kwa mtu kujua wanapitia vikwazo vingapi. Divana usisononeke, tupo na wewe! Ila Gwiji Kassim, kama kuna chako hujapewa kitakuja na utakipata.


The Leader.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger