Ticker

6/recent/ticker-posts

Haji Manara "Mimi Bado ni Msemaji wa Yanga Mpaka Watakapofanya Hili"Siku kadhaa baada ya Kamati ya Maadili ya TFF kumfungia msemaji wa Yanga, Haji Manara kufungiwa kutojihusisha na soka kwa miaka 2 na faini ya Sh20 milioni kwa kukutwa na hatia ya kumtolea maneno yasiyofaa rais wa TFF, Wallace Karia leo amefunguka kwa undani sakata zima na kukataa hukumu hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo Manara amesema;

"Nakala ya hukumu sijapata, mpaka pale nitakapopata na haki ya majibu ya malalamiko yetu ya msajili na Baraza la Michezo (BMT) juu ya kutosajiliwa kanuni na mpaka pale tutakapopata haki ya kukata rufaa mimi bado Msemaji wa Yanga, hukumu haiwi hukumu mbele ya vyombo vya habari kwa mujibu wa taratibu lazima nipate nakala, sijapewa mimi bado msemaji na nitaendelea kufanya shughuli za Yanga hadi pale nipate nakala ya hukumu na kupata majibu ya BMT,"

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments