Ticker

6/recent/ticker-posts

Mama Dangote Ampongeza Diamond Platnumz Kwa Kununua Ndege yake Binafsi Private Jet


Mama mzazi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Bi Sandrah maarufu Mama Dangote, amempongeza kijana wake kwa kununua ndege yake binafsi (Private Jet).


@mama_dangote ambaye hivi karibuni alitoka kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, ametumia insta story yake kutoa pongezi hizo pamoja na kumshukuru Mungu kwa jambo hilo kubwa alililolifanya mwanae, "Allhamdulilaah­čĄ▓, M/mkubwa Leo hii Unamiliki Ndege Naseeb @diamondplatnumz " - ameandika Mama Dangote.


Ikumbukwe, Diamond kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni na DW nchini Ujerumani, amethibitisha kuwa amekwisha nunua ndege yake hiyo binafsi. Na kwenye mahojiano yake mengine ya miezi miwili iliyopita akiwa nchini Ivory Coast, alisema ndege hiyo itatua nchini kabla ya mwezi Oktoba.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments