Ticker

6/recent/ticker-posts

Mfahamu Kiundani IGP Mpya Camilius Wambura, Mrithi wa Simon SirroWote tunafahamu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi ambapo amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP akichukua nafasi ya Simon Sirro.

Nimejawa na furaha kuona mtu makini ndani ya Jeshi la Polisi mwenye uzoefu na weledi anakabidhiwa majukumu makubwa ya kuliongoza Jeshi letu la Polisi. Hakika CAMILIUS WAMBURA ni mtu sahihi mno.

Wengi wetu tunaofuatilia utendaji wa Jeshi la Polisi nchini tulitegemea mabadiliko kufanywa hususani katika nafasi hii muhimu ili kupatikana mtu anayeendana na kasi na dira ya serikali ya awamu ya sita.

Baadhi ya nyadhifa na majukumu ndani ya Jeshi la Polisi yaliyowahi kufanywa na IGP CAMILIUS WAMBURA ni pamoja na;


1. Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi – KINONDONI

2. Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi- Makao Makuu

3. Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA


4. Kamanda wa Polisi -Kanda Maalum-DAR ES SALAAM

5. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

6. Na sasa INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP)

BAADHI YA SIFA ZA KIPEKEE ZA IGP WAMBURA KATIKA UTUMISHI


1. Mpenda haki na muwajibikaji

2. Msomi na mwanataaluma mbobezi ndani ya Jeshi la Polisi

3. Kamanda wa Polisi anayependa kujihusisha na mambo ya kijamii.

4. Mzalendo na mchapakazi katika majukumu mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi

5. Kamanda wa Polisi asiye na makuu na mwenye weledi katika nafasi anazo aminiwa.


Pongezi za dhati kwa IGP CAMILIUS WAMBURA, watanzania na hata Makamanda wenzio ndani ya Jeshi la Polisi ni mashuhuda wa uwezo wako na uwajibikaji tunakutakia utendaji mwema.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments