Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwalimu Amnyonga mkewe na Kujinyonga Mwenyewe GestMwalimu wa Shule ya Sekondari Tanga, Emmanuel Jerome (32), anadaiwa kumnyonga mke wake, Lucy Nshoma (34) katika nyumba ya kulala wageni mkoani Rukwa, kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kamba juu ya mti siku moja baadaye mkoani Katavi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame ameviambia vyombo vya habari kuwa marehemu ni mkazi wa mkoa wa Tanga na kwamba chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi. Kamanda Makame amesema marehemu Jerome alikua na mgogoro na mke wake, ambapo alimtuhumu kutoka kimapenzi na wanaume wengine.


Amesema Jerome na mkewe walipanga safari kuelekea mkoani Rukwa, ambapo ni nyumbani kwao marehemu mke wake na walifikia nyumba ya kulala wageni Julai 26, 2022, ndipo usiku alipochukua uamuzi wa kumnyonga mkewe.

Kamanda Makame alisema baada ya kumnyonga katika nyumba hiyo ya wageni, aliacha ujumbe wa maandishi kwa ndugu wa mke wake uliosomeka: "Nisameheni kwa yaliyotokea". 


Alieleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo mkoani Rukwa alikimbilia mkoani Katavi na Julai 27,2022 usiku, eneo la mtaa wa Ilembo, Manispaa ya Mpanda, alichukua uamuzi wa kujinyonga na walikuta mwili wake ukiwa unaning’inia kwenye kamba.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments