Ticker

6/recent/ticker-posts

Nchimbi anukia Tanzania PrisonsNchimbi katika msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na Geita Gold baada ya kutemwa na Yanga, japokuwa hakuwa na nafasi kubwa ya kucheza kutokana na majeruhi.
nchimbi pic
Winga wa zamani wa Yanga na Geita Gold, Ditram Nchimbi anatajwa kujiunga na Tanzania Prisons iliyonusurika kushuka daraja ili kuongeza nguvu kikosini.

Prisons ilibaki Ligi Kuu kufuatia ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Play Off, ambapo Ijumaa ya wiki hii itakuwa kambini kujiandaa rasmi na msimu ujao.

Hata hivyo timu hiyo ya jijini Mbeya ipo kwenye mawindo ya kusaka nyota nane wapya ikiwa ni makipa wawili, Straikia, beki wa kati na winga mmoja akiwa na jukumu la kutengeneza krosi za mabao.

Chanzo cha ndani ya klabu hiyo, kimeidokeza Mwanaspoti Online kuwa nyota huyo aliyewahi kuzitumikia timu kadhaa ikiwamo Mwadui, Polisi Tanzania, Yanga na Geita Gold huenda akamalizana nao muda wowote.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments