Ticker

6/recent/ticker-posts

R. Kelly aondolewa kwenye uangalizi maalum

Mwimbaji staa wa R&B Robert Sylvester Kelly maarufu R. Kelly ambaye hivi juzi amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 30, ameondolewa kwenye uangalizi maalum aliokua amewekwa gerezani kumuepusha kujiua.

Imeelezwa kwamba R.Kelly aliwekwa kwenye uangalizi huo kutokana na kuwa kwenye hatari ya kutaka kujiua kutokana na msongo wa mawazo uliotokana na mashtaka ya kuwadhalilisha kingono Wanawake na Wasichana yaliyopelekea ahukumiwe kifungo cha miaka 30 katika gereza la Brooklyn, New York.

Waendesha mashtaka hapo awali walisema Mwimbaji huyu mwenye umri wa miaka 55 alihitajika kuwekwa kwenye uangalizi huu maalum kwasababu ya usalama wake lakini Mawakili wake walifungua kesi siku ya Ijumaa wakidai aliwekwa kwenye lindo hilo maalum kama adhabu na sio kusaidiwa.

Uangalizi huu maalum maarufu ‘Suicide watch’ hufanywa kwa Mgonjwa au Mfungwa ambaye yupo katika hatari ya kujiua.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments